Dola Indidis

in #history8 years ago

Kutana na Dola Indidis, mwanasheria aliyeishtaki Israel kwa kumuua Yesu). nadai hakuipeleka kesi mahakamani kwa misingi ya kidini bali kwa misingi ya Kisheria. Anasema "Its academic thing not a theological thing" Yeye anachoangalia si unabii bali legal procedure.

Pia amesisitiza ameamua kumtetea Yesu kama mtoto wa Yusufu (fundi seremala) na sio Yesu kama Masihi "I look Jesus as son of Joseph not as the Messiah"

Alipoulizwa mbona ilitabiriwa Yesu atakufa, anasema anafahamu hilo ila hoja sio Yesu kufa, hoja yake ni process iliyotumika kumuua haikuwa sawa kisheria. Anadai mahakama ilikosea kujiingiza kwenye kesi hiyo "The court should not involve itself in that crooked case."

Anasema Yesu ungehukumiwa kifo kwa kufuata taratibu za kisheria kusingekuwa na shida, ila aliuawa kikatili bila kupewa haki ya kusikilizwa. Wakati Yesu anpelekwa mahakamani (kwa Pilato) tayari alishaanza kusulubiwa kabla hata hukumu haijatoka.

Huo ulikuwa ukiukwaji wa sheria maana mtuhumiwa hawezi kuadhibiwa kabla ya mahakama kujiridhisha kuwa mtu ana hatia. "no punishment could be made unless the court proved beyond the reasonable doubts that Jesus was guilt" Anasema Yesu angepata wakili wa kumtetea angeachiwa huru. Hata kama ilimpasa kufa angeuawa kwa namna nyingine.

Anadai pia Pilato hakuwa na nguvu ya kisheria ya kusikiliza ile kesi na hata yeye alikiri hilo ndio maana akawarudisha wayahudi kwa Herode. Lakini akalazimishwa kutoa hukumu kwa pressure ya mfalme Herode. "Pilate had no jurisdiction to give the judgment, he confessed, and also he confessed the innocence of Jesus"

Pia anadai Pilato alikiri Yesu kutokuwa na hatia, lakini bado alisulubiwa. Sasa kama Pilato ndio alikuwa Jaji na hakuona hatia ya Yesu kwanini bado Wayahudi walimsubisha?

Akaongeza kuwa kitendo cha Wayahudi kumsulubisha Yesu mbele ya Jaji (Pilato) ni kujichukulia sheria mkononi na ni uvunjifu wa haki za binadamu. "Jesus was tochered in-front of Judge, that is abuse of Human rights"

Anadai misingi ya haki ilikiukwa katika kuongoza kesi (miscourage of Justice) na Yesu hakupewa nafasi ya kusikilizwa japo alikuwa akilalamika. "Even Jesus complained but he was not given right to be heard,that is mis-courage of justice."

Amesema pia kuwa maamuzi hayakuzingatia principle of natural justice, na hukumu inapaswa kurekebishwa na Israel kuomba msamaha. "The judgment was bad in law and should be quashed"

Ametumia kesi ya Mwai Kibaki vs Daniel Arap Moi 1999 kama refference ya kesi yake (MWAI KIBAKI Vs DANIEL TOROITICH ARAP MOI, Case Number :Civ App 172 of 1999").

Anaungwa mkono na makanisa kutoka nchi za Norway, Marekani, Israel, Uingereza, Tanzania, Afrikakusini

Coin Marketplace

STEEM 0.27
TRX 0.21
JST 0.038
BTC 96819.40
ETH 3702.03
USDT 1.00
SBD 3.87